WALIMU WAMUOMBA WAZIRI NDALICHAKO KUTATUA TATIZO LA UPUNGUFU WA WALIMU
Walimu nchini wamemwomba Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi,Prof.Joyce Ndalichako kutatua tatizo la ukosefu wa walimu kwani wamekuwa wakifundisha vipindi vingi hivyo kujikuta wakirudi nyumbani wakiwa wamechoka.
Wakisoma risala yao mbele ya Waziri huyo katika
ufungaji wa mafunzo ya walimu wanaofundisha darasa la tatu na nne juu ya Mtaala
mpya unaozingatia ukuzaji wa umahiri wa Stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu
(KKK).
Eda Chilimo kutoka wilaya ya bahi akisoma risala hiyo kwa
niaba ya walimu wenzake kutoka katika Wilaya za Bahi, Kondoa na Dodoma
Mjini,amesema changamoto kubwa wanayokabiliwa nayo ni kufundisha vipindi vingi
kutokana na uhaba wa walimu.
Kwa upande wa Waziri Ndalichako amekiri Tanzania kuwa
na uhaba wa walimu na kuahidi kulitatua tatizo hilo kwa kuwapeleka katika shule
zingine walimu wa ziada.
Kutokana na hali hiyo Waziri Ndalichako, amewaagiza
Wakurugenzi wote nchini kuangalia jinsi ya kusawazisha hali hiyo, pia waziri Ndalichako
amesema Kuhusina na madarasa amesema Serikai imejenga madarasa 1089 huku
ikikarabati shule kongwe 88 lengo likiwa ni kuendeleza elimu nchini.
Hatahivyo, Ndalichako amewataka Walimu hao
kutowanyima wanafunzi vitabu vilivyotolewa na serikali kwani lengo ni wanafunzi
hao wajue kwa ufasaha KKK tatu ambazo ni kusoma,Kuandika na Kuhesabu.
Na Jacquline Victor- Salvanews
Post a Comment