Header Ads

header ad

WAFUASI WA LIPUMBA WADAIWA KUVAMIA MKUTANO WA VIONGOZI WA CUF NA WANAHABARI




Mkutano wa baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kinondoni na waandishi wa habari uliofanyika leo Aprili 23,2017 katika Ukumbi wa Hoteli ya Vina iliyopo maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam umevunjika baada ya kuvamiwa na kundi la watu lisilojulikana linalodaiwa kuwa wafuasi wa Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Akielezea taarifa hizo, Mwenyekiti wa CUF wilayani Kinondoni, Juma Nkumbi amedai kuwa mara baada ya kuanza kuzungumza katika mkutano huo, ghafla walivamiwa na watu waliokuwa wamefunika nyuso zao na kuanza kuwapiga kwa mikanda na mapanga.

“Tukiwa na mkutano wetu na waandishi wa habari eneo la mabibo kwenye ukumbi wa Vina Hotel wakati naendelea kuongea ghafla kuna kundi kubwa la watu wakiwa wamevaa ninja likaingia ndani na kuanza kutupiga kwa mikanda na mapanga na kuumiza watu wetu pamoja na waandishi wa waandishi habari baada ya kujitetea wakashuka chini,” amesema na kuongeza.

“Kule chini walikuwa na magari mawili aina ya Landcruzer na Coster moja yenye bendera za CUF tukapiga kelele wananchi wakatusaidia kuwafukuza wakakimbia hawa wanatoka buguruni ni wafuasi wa Lipumba ambao hataki huku Bara tuseme ukweli kuhusu hali halisi ya chama chetu.”
Amesema baada ya tukio hilo kutokea walitoa taarifa katika kituo cha Polisi cha Magomeni na kwamba hadi muda huu askari polisi wako eneo la tukio

No comments

Powered by Blogger.