Header Ads

header ad

UHAMIAJI WAZINDUA MFUMO WA UHAKIKI WA KIELEKTRONIKI

 Na James Salvatory 
Idara ya uhamiaji imezindua mfumo wa uhakiki wa vibali vya ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki"e-verification" ukiwa na lengo la  kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi hapa nchini pamoja na kuzuia mianya ya upotevu ya maduhuli  ya serikali .
Akizungumza na wandhi wa habari jana Jijini Dar es salaam Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala, alisema kuwa kampuni, Taasisi  na Mashirika binafsi baada ya kuhakiki vibali vya wageni wao kupitia mfumo huo watatakiwa kuwasilisha taarifa za vibali hivyo katika ofisi za uhamiaji za mikoa zilizopo katika maeneo yao      
Katika hatua nyingine idira ilitoa wito kwa waajiri, wamiliki wa makampuni na wote wenye vibali  vya kukaazi kutoa ushirikiano katika kipindi chote cha zoezi  na idara inawaomba wadau wa huduma za kiuhamiaji kufika wao wenyewe katika ofisi zao  zilizopo nchini kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na makao makuu
Kuanza kwa mfumo huu wa uhakiki wa vibali vya ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki "e-verification" kupitia  tovuti ya www.immigration.go.tz , idara imetoa muda wa siku  tisini ili kuhakiki taarifa za vibali  vya wageni  na baaada ya muda  huo kwa wale ambao watakuwa hawajahakiki vibali vyao hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa.
Powered by Blogger.