Header Ads

header ad

NMB YAKABIDHI SEHEMU YA KUMPIZIKIA WAGOJWA MUHIMBILi




Na James Bayachamo-Salvanews

Benk ya NMB  yakabidhi Jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao wanaowaleta wagonjwa kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.


Akizungumza jana wakati wa kukabidhi  jengo hilo Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo lenye uwezo wa kuhifadhi watu 100 kwa pamoja wakiwa wamekaa kusubili  huduma na  ni sehemu ya huduma za kijamii zinazoilenga sekta ya afya ambapo benki hiyo imeweka utaratibu wa kusaidia.

Amesema kukamilika kwa jengo hilo la kupumzikia kutasaidia wagonjwa wa nje na ndugu zao ambao hufika kupata huduma JKCI kupumzika sehemu tulivu na salama huku wakisubiri kuhudumiwa na madaktari wa kituo hicho bila kero. Alisema msaada huo NMB inaamini imeutoa kwa wateja wao pia ambao nao hufika na kupata huduma katika hospital


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na wanahabari kabla ya kuzinduwa jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa.

Aidha, Bi. Bussemaker amesema  kuwa Benki ya NMB kwa mwaka 2017 imejipanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni moja kusaidia huduma za kijamii hususani katika sekta ya afya, elimu pamoja na kusaidia majanga mengine yanayoikumba jamii na Kwa mwaka 2016 benki hiyo ilitumia takribani milioni 260 nchi nzima kusaidia vifaa mbalimbali vya hospitalini huku jumla ya hospitali 33 zikinufaika kwa msaada huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi aliishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo na kudai hii sio mara ya kwanza kwa benki hiyo kuisaidia JKCI katika s
hughuli zake. Alimpongeza msaada huo ni mkubwa kwao na unajenga mazingira mazuri ya huduma kwa wateja wao hivyo kuishukuru sana NMB pamoja na uongozi na wafanyakazi wake.

No comments

Powered by Blogger.