kutekwa kwa Ben saanane UTG wazidi kulia na vitendo vya utekaji
UMOJA WA KIZAZI CHA KUHOJI TANZANIA WALIA NA VITENDO VYA UTEKAJI, UPOTEAJI NA MAUAJI YA RAIA.
Na James Salvatory,
Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Tanzania (UTG), umeliomba jeshi la polisi kutangaza oparesheni maalumu ya kukomesha vitendo vya utekaji, upoteaji na mauaji ya raia nchini sambamba na kutoa taarifa ya mwenendo wa uchunguzi katika suala la kupotea kwa Ben Saanane.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa taasisi ya UTG Godlisten Malisa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ikiwa ni mwendelezo wa harakati za umoja huo kushinikiza kupatikana kwa katibu mkuu wa taasisi hiyo Ben Saanane ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu mwezi november mwaka jana ambaye mpaka sasa haijulikani alipo.
Amesema kuwa kutokana na vitendo hivyo, UTG imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kuwasilisha malalamiko rasmi (ya maandishi) kwa tume ya haki za binadamu na utawala bora ambayo kikatiba ina mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.
Ameongeza kuwa kutokana na vitendo hivyo,UTG imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kuwasilisha malalamiko rasmi (ya maandishi)kwa tume ya haki za binadamu na utawala bora ambayo kikatiba ina.mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.
Kwa upande wao
Agripina Saanane na Erasto Saanane ni ndugu zake na Ben Saanane wao
wameshukuru jitihada za watu mbalimbali ikiwemo wandishi wa habari,
wambunge wananchi katika kuhakikisha kaka yao anapatikana.
Katika hatua nyingine
UTG) imeliomba bunge la Jamuhuri ya mMuungano wa Tanzania kujadili hoja
kuhusu kudorora hali ya usalama nchini kufuatia matukio ya kupotea,
kutekwa na kuuawa kwa baadhi ya watanzania katika maeneo mbalimbali
nchini huku ikitoa pole kwa jeshi la polisi na familia za askari wanane
waliopoteza maisha wilayani Kibiti mkoa wa Pwani baada ya kushambuliwa
na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Post a Comment