Header Ads

header ad

JPM MGENI RASMI KONGAMANO LA MAADILI LILILO ANDALIWA NA BAKWATA


Image result for picha za shekh mataka wa bakwata

Na Maria Kaira

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kongamano la mmomonyoko wa maadili katika jamii, linalo tarajiwa fanyika April 24 mwaka huu katika ukumbi wa mwalimu Nyerere Jiji Dar es salaam,kuanzia Majira ya Saa 3 likiwa  na lengo la kurejesha maadili katika jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Mwenyekiti wa halmashaul kuu Sheikh Hamis Mataka amesema kongamono hilo limeandaliwa na Baraza kuu la waislamu (BAKWATA)na litakuwa la siku moja .

Pia Sheikh Mataka amesema katika kongamano hilo litaudhuliwa na masheikh wa mikoa mbalimbali,masheikh kutoka taasisi mbalimbali, mabalozi wa nchi mbalimbali, wakuu wa vyombo vya usalama pamoja na wananchi wote.

"Jamii yoyote inayotaka kuendelea lazima iwe na maadili mema unapoona Jamii inasumbuliwa na ulevi, wizi madawa ya kulevya hiyo ni sehemu moja wapo ya mmomonyoko wa maadili katika jamii haiwezekani Binadamu mwenzio anapata ajali unaanza kumsachi na kumwibia badala ya kumuokoa" amesema

Aidha sheikh Mataka amesema katika  kongamano hilo linatarajia kufungwa na Rais wa Zanzibar Dr. Ally Mohammed Shein.

"Kongamono  hili litakuwa na masheikh watatu ambao wata
wasilisha mada mbalimbali akiwemo sheikh Suleiman Kilemile ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wanazuoni wa kiislam yeye atazungumzia mmomonyoko wa maadili katika jamii, katibu wa mufti zanzibar sheikh Fadhili atazungumzia umuhimu wa ujenzi wa familia na jamii salama, Pia kutakuepo na Dkt atakayezungumza juu ya madawa ya kulevya na madhara yake pamoja na Takwimu kwa ujumla zinasemaje" amesema
Powered by Blogger.