JESHI LA POLISI DODOMA LASEMA LIKO IMARA SIKU YA SHEREHE ZA MUUNGANO
Jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola limesema kuwa lime,jipanga kikamilifu maeneo yote ya mji wa dodoma kwa kuimarisha ulinzi ,doria na msako katika kuhakikisha maadhimisho ya sherehe za muungano yanafanyika kwa amani na utulivu.
Jeshi hilo limesema kuwa mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa ambayo imepewa heshima kubwa kitaifa kwa kufanya maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 53 ya muungano yatakayo fanyika kesho april 26 mwaka huu, hivyo wageni wa ndani na nje ya nchi wanatarajia kufika mkoani hapa kwa maadhimisho ya sherehe hiyo, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “MIAKA 53 YA MUUNGANO; TUULINDE NA KUUIMARISHA; TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII”.
pia jeshi hilo limeongeza kuwa litahakikisha wageni wote wanasherekea kwa amani na utulivu, pia limewataka wenyeji wa dodoma kutumia fursa kwa kufanya biashara na kutoa huduma bora kwa wageni watakao fika.
Wakati huo huo jeshi hilo limethibitisha kukamatwa kwa silaha aina ya Gobole yenye No. MP.0059/2000 iliyotengenezwa kienyeji huko kijiji cha IBWAGA kata ya Ugogoni wilaya ya Kongwa, ambapo mtuhumiwa ametajwa kuwa ni DAVID NJOHOLE, aliyetoroka kabla ya kufanyiwa upekuzi, na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na makosa ya unyang’anyi, uvunjaji na uporaji wa pikipiki katika vijiji vya wilaya ya Kongwa, ambapo msako mkali unaendelea.
Hatahivyo, jeshi la polisi, limewataka wananchi mkoani hapa kushirikiana kwa pamoja kufichua makundi ya wahalifu yanayo panga kufanya uhalifu,
Post a Comment