Header Ads

header ad

MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA


Kufuatia *Mazungumzo Marefu ya Kina* baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mhe. PAUL MAKONDA* na *Uongozi wa Clouds Media* ameridhia kuongeza *Masaa Machache ya Tamasha la Fiesta* kwenye Viwanja vya Leaders Club *ili kuruhusu Wasanii Wote kutumbuiza*. 

Katika Mazungumzo hayo *RC MAKONDA* aliwataka Clouds *kuchagua Kati ya kufanya Tamasha hilo kwenye Uwanja wa Uhuru ili wapige Mziki hadi Asubuhi au kufanya kwenye Viwanja vya Leaders Club Clouds* ambapo Clouds walichagua kufanya Tamasha hilo *Viwanja vya Leaders Club* na wapo tayari kufuata *Sharti la kutoongeza Muda waliokubaliana.* 

Aidha *RC MAKONDA* amesema kuwa baada ya Tamasha *Hatoruhusu tena Viwanja vya Leaders Club kutumika kwa Matamasha ya Usiku kwakuwa ni Usumbufu wa Wakazi na Ofisi za Bilozi zilizopo jirani na Viwanja hivyo.*

Amesema kuwa Viwanja hivyo kwa sasa vitatumika kwa *Matukio ya Nyakati za Mchana pekee* hivyo kwa anaetaka kufanya Tamasha la kukesha atumie *Uwanja wa Uhuru* ambao umefunikwa na haupo karibu na Makazi ya Watu. 

Amewataka Wananchi kufuata *Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali* na kusisitiza kuwa *Sheria haina upendeleo kwa yoyote.* 

Amewasihi Wadau wa maendeleo kuwekeza katika *Ujenzi wa Kumbi kubwa zenye Soundproof na uwezo wa kubeba watu Wengi* ili zitumike kwenye matamasha ya kukesha.

No comments

Powered by Blogger.