Header Ads

header ad

POLISI DAR WAZUIA MAOMBI YA VIJANA WA CHADEMA



Kamanda wa polisi  kanda maalumu ya dar es salaam Lazaro Mambosasa  akizungumza na wandishi wa habari Leo jijini dar es salaam





makamu  Mwenyekiti wa bavicha kitaifa Patrick Sosopi akizungumza na wandishi wa habari mapema Leo jijini dar es salaam



Baraza la vijana chadema (Bavicha) limesema  kuwa  litafanya ibada ya   maombezi ya kitaifa siku ya jumapili katika  maeneo ya Sinza darajani yakiwa  na lengo la kumuombea Lissu na watu wengine ambao walishawahi kupata kadhia kama hiyo

Akizungumza na wandishi wa habari Leo jijini dar es salaam makamu  Mwenyekiti wa bavicha kitaifa Patrick Sosopi amesema kuwa  wao hawakwendi kufanya siasa Bali wataenda kufanya maombi yatakayojumuisha dini 
Aidha amesema kuwa     

Kwa Upande wake Jeshi la polisi kanda maalimu ya dar es salaam limesema halitaruhusu  maombi ambayo yalipangwa kufanyika siku ya jumapili na vijana wa chadema (bavicha) na Yale maandamo ya cuf siku ya jumatatu huku wakizuia  kusanyiko lolote lile la kimaombi la na  badala yake watumie nyumba za ibada kufanya hivyo ikiwemo msikiti au Kanisa vinginevyo itahesabika ni mkusanyiko na hatua zitachukuliwa.                     

Awali akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa polisi  kanda maalumu ya dar es salaam Lazaro Mambosasa  amesema Majambazi watatu wameuawa  Mara baada ya  kujeruhiwa wakati wakikimbizwa   hospitali ya taifa Muhimbili ili kupatiwa matibabu,
na askari walianza kufyatua risasi kuwashambulia askari na ndipo askari walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu kati ya watano huku wengine wawili wakikimbia.


Aidha Mambosasa amesema kuwa wamefanikiwa  kukamata silaha moja bastola aina ya BERRETA yenye namba A065775Z ikiwa na risasi tano ndani ya magazine katika majibizano ya risasi kati ya askari polisi na majambazi wapatao watano(05).

Na James Salvatory

No comments

Powered by Blogger.