Header Ads

header ad

KITUO CHA UTAMADUNI WA INDIA CHALETA MBADALA WA DAWA

Kituo cha Utamaduni wa India nchini kimezindua mradi wa Dawa za asili ambazo zitaweza kutatua matatizo ya magonjwa mbalimbali nchini.

        Akizungumza na waandishi wa habaribjijini Dar es Salaam Balozi wa India Nchini Mh.SANDEEP ARYA amesema kuwa mifumo ya AYUSH ni kiini kinachoshughulikia tiba ya afya na ustawi,mifumo yao na maudhui yake na bidhaa zao.




         Aidha Mh.SANDEEP amesema kuwa moja wapo ya dawa za asili ni AYURVEDA ambayo inahusika na mambo ya kimwili,kisaikolojia,kiroho na kijamii ya maisha na mgawanyiko wake katika sehemu nane wa utaratibu za matiba0bu huingizwa chini ya panchkarma kuepuka na kuzuia visababishi vya magonjwa na vyanzo vya ugonjwa,utakaso na tabia ya maisha..




             Kwa upande wake Mwalimu wa YOGA Mh.BHARAT SINGH amesema YOGA ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye asili katika  falsafa ya Uhindi kwa miaka mingi na vilevile inajumuisha umoja wa roho na mwili,mawazo na matendo,kujizuia na kujiridhisha ,uelewano kati ya mwanadamu na mazingira yanayomzunguka pamoja na mtazamo wa kiujumla wa afya ya binadamu.


No comments

Powered by Blogger.