Header Ads

header ad

ZAIDI YA ASILIMIA 50 YA WATOTO WANAOZALIWA NCHINI HAWANYONYESHWI IPASAVYO

Zaidi ya asilimia 50  ya watoto wanaozaliwa nchini hawanyonyeshwi maziwa ya mama kwa kipindi kinachoshauriwa kitaalamu  hali inayosababisha kupatwa na madhara mbalimbali ya  kiafya kama vile udumavu wa mwili na akiri,kuharisha,na kushambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara.


Hayo ni kwa mujibu wa Daktari bingwa wa Watoto kutoka Hospitali ya Agha Khan  iliyopo jijini Dar es salaam,Bi.Mariam Nooran wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi wa video inayohusu utoaji wa elimu juu ya unyonyeshaji wa maziwa bora.

Aidha Dr.Nooran amesema kuwa unyonyeshaji unaotakiwa kiafya ni kunyonyesha kwa muda wa miezi sita maziwa ya mama bila kumlisha mtoto chakula mbadala na kudai kuwa endapo mtoto hatanyonyeshwa maziwa ya mama kwa kipindi cha miezi sitaanaweza kupatwa na madhara mbalimbali ya  kiafya.

Dkt.Lucy Hwai ni muuguzi mkuuu wa hospitali ya Agha Khan anaelezea kuwa mikakati ya hospitali hiyo ni kuendeleza mpango wa kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa kutoa elimu mapema kabla ya kujifungua katika kliniki za wajawazito na eneo la kusubiri huduma.

Hata hivyo Bi.Pamela Slemani mmoja wa wakina mama wanaonyonyesha waliyohudhulia uzinduzi huo wakiambatana na waume zao,amesema kuwa wakina mama wengi hawapati ushauri na elimu kutoka kwa wataalam, ili kutambua aina ya vyakula ambavyo husaidia kutoa maziwa ya kumtosha mtoto.
.


Uzinduzi wa Video ya elimu ya unyonyeshaji, pia umeenda sambamba na uzinduzi wa group la mtandao wa kijamii kama vile“WATSAAP” litakalotumika kupashana  habari za kiafyaa z kwa urahisi.


Na James Bayachamo-Salvahabari

No comments

Powered by Blogger.