MANENO YA SUMUMAYE KWA SERIKALI KUHUSU MASHAMBA YA FAMILIA YAKE
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Sumaye ameeleza kuwa licha ya mahakama kuu kuweka zuio la muda (court injuction) kuhusu mashamba mawili ya familia yake la Mabwepande jijini Dar es Salaam lenye ekari 33 linalomilikiwa na mtoto wa Sumaye ndugu Franklin Sumaye na lingine la MvomeroMkoani Morogoro lenye ekari 326 linalomilikiwa na mke wake Sumaye Esther Sumaye, serilaki imekaidi agizo hilo la mahakama na kulitwaa shamba hilo ili wavamizi waendelee kuishi maeneo hayo kinyume cha sheria, alieleza Sumaye.
Sumaye ameongeza kuwa hawezi kuchukua hatua yeyote kwasasa anasubiri maamuzi ya mahakama juu ya kesi hiyo ambayo bado inaendelea lakini ikitokea ameshindwa kesi hiyo atamuachia Mwenyezi Mungu.
"Mimi sing'ang'anii hayo mashamba ninachokiomba haki itendeke lakini serikali imeingilia majukumu ya mahakama na kulitwaa shamba wakati kesi inaendelea mahakamani hili jambo siyo sahihi kabisa kwa nchi yenye kufuata utawala bora" Alieleza Sumaye.
Sumaye amefunguka zaidi na kueleza kuwa serikali ikiendelea kufanya maamuzi bila kuzingatiia sheria itaendelea kulipa fidia na kuliingiza taifa katika hasara, kwasababu kesi zikienda mahakamani serikali lazima ishindwe.
Post a Comment