MANAIBU WAZIRI WATATU WATEMBELEA UJENZI WA JENGO JIPYA LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA JNIA JIJINI DAR ES SALAAM
Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Abiria wa Forodha kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Damas Temba (wa kwanza kulia), akitoa maelezo kwa Manaibu wa Wizara za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Mhandisi Edwin Ngonyani (wa kwanza kushoto), Wizara ya Maliasili na Utalii – Mhandisi Ramo Makani (mwenye miwani) na Wizara ya Mambo ya Ndani – Mhe. Yussuf Masauni (wa tatu kulia) walipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya JNIA.
Imeelezwa kuwa Ufinyu na uchache wa watumishi kwa baadhi ya idara zinazotoa huduma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere unasababisha kuchelewesha kwa abiria wa kigeni wanaotumia uwanja huo.
Haya yamebainishwa leo wakati wa majadiliano ya manaibu mawaziri wa tatu wa nchini yaani Mambo ya ndani, mali asili na utalii na ujenzi uchukuzi na mawasiliano pamoja na wadau wanaotoa huduma katika uwanja huo ambao ni polisi, uhamiaji na mamlaka ya usimamizi viwanja vya ndege (TAA).
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa TAA Mtengela Hanga amesema katika uwanja huo wanapaswa kuwepo maofisa wa uhamiaji 50 kwa kila shifti lakini wapo 30 hivyo kuna upungufu wa watumishi 20.
Kwa upande wao manaibu hao wamebaini changamoto kadhaa katika kiwanja hicho na kile cha kipya kinachoendelea kujengwa na kwa umoja wao wameahidi kutatua matatizo waliyoyabaini hususasi upande wa jeshi la uhamiaji, huku wakiahidi kuendelea na ukaguzi bandalini na kwenye mipaka yote ya Tanzania.
kutokana na changamoto hizo abiria huhudumiwa chini ya muda wa kimatiafa, huku Abiria moja huhudumiwa kwa masaa matatu badala ya dakika 45 kwa kila abiria.
Na James Salvatory
Post a Comment