TCRA YAZUIA MAKAMPUNI YA SIMU KUTOA MATANGAZO KWENYE HUDUMA ZA MAWASILIANO
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka makampuni ya simu kusitisha Mara moja utoaji wa matangazo kwenye huduma za mawasiliano.
Akizungumza mapema Leo jijini dar es salaam mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo James Kilaba amesema kuwa Tcra imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wa mawasiliano, wakionesha hisia zao kwa kukerwa na huduma za matangazo yanayotolewa na watoa huduma wakati wa kupiga simu hususani kabla ya simu kuita,kujiunga na huduma za miito ambazo hutokea kabla ya kumuunganisha mpiga simu na Yule anayempigia na Yale yanayoyoletwa wakati wa mtu unavyompigia simu na kukuta anaongea na simu nyingine au hapatikani kwa wakati huo.
Aidha Kilaba amesema sambamba na matangazo hayo pia watoa huduma wamekuwa wanatoa matangazo kwa njia ya ujumbe mfupi(SMS) bila ya ridhaa ya wateja ambapo ni kinyume cha matakwa ya kanuni za huduma za ziara (VAS Regulations) za mwaka 2011 huku kwa upande wa kupiga simu matangazo hayo hutangulia kumpa mpigaji ujumbe wa matangazo kabla ya kumpatia huduma muhusika na hivyo kumpotezea muda na hutolewa bila ya ridhaa ya muhusika
Kwa mujibu wa kanuni za huduma za ziada (VAS Regulations) mwaka2015 kampuni ya simu inatakiwa kutoa taarifa kwa ukamilifu kwa kingireza au kiswahili, kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni za kumlinda mtumiaji wa huduma za mwaka 2011;kanuni ya 8(1),kutoa matangazo na taratibu za kujiunga na huduma mbalimbali za ziada wakati wa kumjibu mteja anapoulizia Salio la muda wa maongezi, mteja anapopokea taarifa baada ya kuongeza Salio na mteja anapoingia kwenye orodha ya huduma za mtoa huduma kanuni ya 8(2) na hairuhisiwi kutoa matangazo mengine yoyote kwa njia za mawasiliano ya simu au njia yoyote ya kielektroni bila kuzingatia vigezo vilivyowekwa.
Na James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment