Header Ads

header ad

TCRA YAZIPIGA FAINI MITANDAO YA SIMU NCHINI

            
                               
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeyatoza faini makampuni sita  ya simu kwa kushindwa kuzingatia utaratibu wa usaijili wa namba wa laini za simu za kiganjani.


Akizungumza Leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Mhandisi James Kilaba, amesema kuwa si mara ya kwanza kwa watoa huduma hao kukiuka sheria kwani wamekuwa  wakisajiri line za simu  kiholela bila  ya kuhitaji vitambulisho kutoka kwa wanunuzi au  wamiliki wapya wa laini za simu.

Aidha Kilaba amesema kutokana na kuathiri na kuhatarisha usalama wa umma na jamii ya Watanzania kwa kusajili laini bila kufuata utaratibu kampuni hizo zimetozwa Sh500 milioni kila moja.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo ametoa wito kwa kila mtu anayehitaji kununua line ya simu kuhakikisha anasajiri kikamilifu kwa kutumia taarifa zake na kwa kutokufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake na aliyehusika kusajili na kampuni ya simu husika .

Kampuni za simu ambazo zimetozwa faini  kutokana na makosa  hayo ni pamoja  na  Airtel, vodacom, Smart, Tigo,Zantel, na Halotel

No comments

Powered by Blogger.