Header Ads

header ad

STARS YAPANDA KWA NAFASI 25 VIWANGO VYA DUNIA


Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza viwango vipya vya soka duniani kwa mwezi Juni ambapo kwa Tanzania hali imekuwa nzuri baada ya kupanda kwa nafasi 25.
Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 139 hadi 114 jambo ambalo linanyesha ni wazi timu ya Taifa imeonyesha kiwango kizuri kwa michezo yake ya hivi karibuni ikiwa chini ya kocha Salam Mayanga.
Nafasi ya kwanza kwenye viwango hivyo imeshikwa na Ujerumani ikipanda kwa nafasi mbili na kuishusha Brazil na Argentina, nafasi ya nne inashikwa na Ureno, Switzerland, Poland, Chile, Colombia, Ufaransa na Ubelgiji ikiwa katika nafasi ya kumi.
Kwa upande wa Afrika, Misri inaongoza ikifuatiwa na Senegal,Congo DRC, Tunisia, Cameroon, Nigeria, Burkina Faso, Algeria, Ghana na  Ivory Coast ikiwa katika nafasi ya kumi.

No comments

Powered by Blogger.