SERIKALI YASHAURIWA HAYA JUU YA UPATIKANAJI WA MAFUTA
Serikali imeshauriwa kuwekeza katika sekta ya mafuta ya kula ili kuweza kuzalisha mafuta mengi zaidi ambayo yataweza kukidhi mahitaji ya watanzania badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi kwani kwa sasa ni asilimia 30 tu ya mafuta yanayozalishwa hapa nchini huku asilimia 70 ikiagizwa kutoka nje.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Sera wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Glead Teri wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam wakati akitoa taarifa za utafiti uliofanywa na wadau mbali mbali wa sekta binafsi pamoja na Seriknchi.
Aidha amesema sekta ya mafuta ya halizeti ina uwezo wa kuwahudumia zaidi ya watanzania milioni 18 na kuwaondoa Katika umaskini,hivyo ipo haja ya Serikali pamoja na wadau Kuandaa mipango madhubuti ya kuweza kuliangalia jambo hili ili kuweza kuleta mabadiliko katika sekta ya mafuta pamoja kuwasaidia wazalishaji wa ndani.
Kwa upande wake mshauri elekezi katika masuala ya kijamii na kiuchumi kutoka kampuni ya Macc Group Ltd,Braison Salisali kutoka Dodoma,amesema kuwa wakulima wengi wanakumbwa na chanagmoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mbegu bora za mafuta pembejeo za kilimo,pamoja na mafunzo hali inayochangia uzalishaji mdogo wa mafuta ya kula.
Naye, Mkurugenzi msaidizi idara ya Viwanda Juma Mwambapa Amesema kuwa, Serikali imeweka mazingira mazuri ya kuakikisha wazalishaji wanaweza kuzalisha bidhaa zao pamoja na kuweza kutuo ajira kwa vijana.
kwa mujibu wa utafiti , ifikapo mwaka 2030 inakisiwa watanzania wanatarajiwa Kufika Mill 82 ambapo watatumia mafuta tani laki saba na nusu, hivyo ipo haja yaekuweza na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mafuta na kupunguza kasi ya uagizaji kutoka nje nchi.
James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment