ONGEZEKO LA WATU LACHANGIA UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU NA HUDUMA KUTOKUTOSHELEZA MAHITAJI
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Otilia Gowele (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya (haupo pichani) alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani iliyofanyika leo katika viwanja vya Mwembe yanga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Dkt. Hashina Begum na kulia ni Mratibu wa Idadi ya Watu kutoka Tume ya Mipango Ibrahim Kalengo.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (wa pili kushoto) Irenius Ruyobya akimuelimisha mmoja wa wananchi waliotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani iliyofanyika leo katika viwanja vya Mwembe yanga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkutubi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Issa Magabiro (wa kwanza kulia) akitoa maelezo juu ya huduma zinazotolewa na ofisi hiyo kwa baadhi ya wananchi wa Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani iliyofanyika leo katika viwanja vya Mwembe yanga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha ngoma cha Malezi Cultural Group kikitumbuiza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani iliyofanyika leo katika viwanja vya Mwembe yanga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA).
Ikiwa leo ni Siku ya Idadi ya Watu Dunia, Imeelezwa kuwa taifa na familia nyingi zinakabiliwa na changamoto ya upungufu ya miundombinu na huduma za kutosheleza mahitaji yanayoongezeka kwa kasi kubwa kutokana na shinikizo la ongezeko la idadi ya watu .
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa Leo jijini dar es salaam katika viwanja vya mwembe yanga temeke, Naibu katibu mkuu wizara ya afya jinsia wazee na watoto Dkt.Otilia Gowelle amesema kila mwaka kuna vijana zaidi ya million 1.2 wanafikia umri wa kuingia katika soko la ajira lakini ni chini ya laki tatu tu ndiyo wanaofanikiwa kuingia katika ajira hali inayosababisha kuwa na wimbi kubwa la makazi holela na kuzuka kwa maeneo ya biashara yasiyokuwa rasimi huku ikishuhudiwa uhamiaji wa vijana kwenda mijini ambazo Hazipo za kutosheleza.
Aidha amesema kuwa pamoja na mafanikio katika sekta ya afya kuna haja ya kuongeza elimu na uhamasishaji juu ya matumizi ya uzazi wa mpango katika taifa na ngazi ya kaya na kwa sasa jamii iko tayari na kuna makundi mbalimbali yanashiriki kupeleka elimu kwa Jamii na kuhamasisha hili na kuna umuhimu wa kupunguza kasi ya idadi ya watu
Naye Afisa habari kutoka Tume ya Mipango werren bright amesema utafiti unaonyesha katika kila Dora moja mpka Dora sita ambayo serikali inayowekeza katika uzazi wa mpango inaweza kuokoa shughuli za maendeleo zikiwemo kupunguza umasikini,elimu na majanga yanayoweza kujitokeza hivyo uzazi wa mpango ukizingatiwa taifa litakuwa katika tija nzuri na kama uzazi wa mpango utafuatwa unaweza kuedeleza uchumi na kuokoa vifo vya wakina mama.
Na James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment