MWIJAGE AAGIZA HAYA KUHUSU WALIOSHINDWA KUENDELEZA VIWANDA
Waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage, amewaagiza wakuu wa mikoa yote kupita kwenye maeneo yao kukagua viwanda vilivyobinafsishwa ili kujua kama vimekufa ama vinafanya kazi ili vioombewe leseni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwijage amesema hatima ya viwanda vilivyobinafsishwa halafu havifanyi kazi itajulika agosti 15 mwaka huu na hatua zitakazochukuliwa kwa viwanda hivyo ni pamoja na kuwanyang’anya wawekezaji hao na kuwapa watu wenye uwezo wa kuviendeleza.
Katikahatua nyingine akizungumzia taarifa za kuwepo kwa mchele wa plastiki amesema mchele huo haupo nchini na kuwataka wanaosambaza picha za mchele huo waende Ofisini kwake ili wakamuoneshe ulipo.
Uhakiki wa viwanda hivyo umekuja siku chache mara baada ya Rais John Magufuli, akiwa Mkoani Singida alipofanya ziara ya kuzindua barabara ya Itigi-Manyoni Chaya na alisema hakubaliani na suala la ubinafsishaji
Na James Salvahabari
Post a Comment