MAKAMBA AWAPIGA CHINI WAJUMBE WA NEMC
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akifafanua jambo mbele yanwaandishi wa habari (hawapo pichani) akitangaza uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) pamoja na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola na kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano wao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) alipokuwa akitangaza uamuzi wa kusitisha uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na wajumbe saba wa Bodi ya baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
………………………………………………………………………….
Waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa raisi muungano na mazingira January Makamba ametengua uteuzi wa wajumbe wote saba wa bodi ya Baraza la taifa la hifahi na usimamizi wa Mazingira (NEMC), na kuwasimamisha kazi Watumishi wanne kwa tuhuma zinazowakabili kuhusu utendaji wao wa kazi.
Akizungumza Leo jijini Dar es salaam, makamba amesema kuwa utendaji wa nemc umekuwa ukilegalega na kutoridhisha kwani kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, wawekezaji wa ndani na nje kuhsu ucheleweshaji na urasimu usiokuwa wa lazima katika mchakato wa tathimini ya athari kwa Mazingira (EIA),tuhuma za rushwa katika mchakato wa ukaguzi na tathimini ya athari kwa mazingira na kutengeneza vyeti ambavyo havijafuata mchakato stahiki ,,kutokuwa na lugha nzuri kwa wateja na kuwatisha ili watoe chochote.
Aidha waziri makamba amesema wamefanya mabiliko kadhaa ya wakurugenzi na wakuu wa kanda za NEMC ambapo Charles Wangwe, mkurugenzi wa fedha na utawala wa NEMC amerejeshwa wizara ya fedha na mipipango kuanzia Leo na wakuu wa kanda za NEMC Wamebadisalaam Jafari Chimgege aliyekuwa kanda ya Mashariki atakuwa mkuu wa kanda ya kati Dodoma na Good love Mwamsojo aliyekuwa kanda ya nyanda za juu mbeya atakuwa mkuu wa kanda ya mashariki Dar es salaam
Katika hatua nyingine Makamba ameziagiza NEMC kuweka bei elekezi na ukomo kwa Consultants kwa kila aina ya miradi inayoyakiwa kufanyiwa EIA na
kuanzia sasa miradi itakayopelekwa NEMC kuombewa cheti cha EIA ni ile ambayo tayari imefanyiwa kazi na washauri elekezi (consultants), hapatakuwa na haja ya kusajiri mradi NEMC Kwanza.
kuanzia sasa miradi itakayopelekwa NEMC kuombewa cheti cha EIA ni ile ambayo tayari imefanyiwa kazi na washauri elekezi (consultants), hapatakuwa na haja ya kusajiri mradi NEMC Kwanza.
Na James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment