WANAFUNZI WALIOFAURU MASOMO YA KEMIA NA BAIOLOJIA WAPONGEZWA NA KUZAWADIWA VYETI
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Mkemi Mkuu wa Serikali Profesa David Ngassapa, Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliozawadiwa kuangalia picha zaidi shuka chini.
Mkurugenzi Mwakilishi wa Vyuo Vikuu vya Nje hapa nchini (Universities Abroad Link Limited Tanzania UAL) Bw. Tony Rodgers Kabetha.
……………………………………………………………………………..
Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala, uongozi wa Wakala wa Mkemia mkuu wa Serikali , Walimu, Wadau mbalimbali wamepongezawa kwa kufanikisha kazi ya kuandaa hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa Kidato cha Tano na Cha Sita mwaka 2015 na 2016 waliofauru vizuri katika masomo ya Kemia na Baiolojia bila kuwasahau, wazazi na wanafunzi wenyewe ambao ndio wamezesha tukio hilo kufanyika kwa mafanikio.
Akisoma Hotuba ya Naibu Waziri wa, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Khamis Kigwangala Mganga mkuu wa Wizara ya Afya Profesa Mohamed Bakari ambaye alimwakilisha Naibu Waziri huyo amewaalika wadau wengine kuhamasisha na kuwezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya sayansi kwa kuwatambua na kuwazawadia Hivyo kuongeza idadi ya wanasayansi na wataalamu nchini.
“Utaratibu huu wa kuzawadia wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biologia utakuwa chachu kwa vijana kuongeza juhudi katika masomo. Hivyo basi ni vema Wazazi na Waalimu ni vema mkaendelea kuwaongoza na kuwatia moyo, pia taasisi, makampuni na Jamii kuendelea kuwahamasisha na hatimaye Taifa liweze kuwa na hazina kubwa ya rasilimali watu, ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya”
Wanafunzi hao wamekabidhiwa vyeti na fedhna ambazo wameingiziwa kwenye akaunti zao zawadi hizo ni kati ya shilingi 500.000, 450.000, 300.000 kulingana na madaraja huku walimu wakizawadiwa kiasi cha shilingi laki 500.00 kila mmoja ili ziwasaidie katika mahitaji yao madogomadogo wakiwa shuleni.
Naye Mkurugenzi Mwakilishi wa Vyuo Vikuu vya Nje hapa nchini (Universities Abroad Link Limited Tanzania) Bw. Tony Rodgers Kabetha ameungana na Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kwa kuwapongeza na kuwatambua wasomi hao wa elimu ya sekondari ambao wamefauru vizuri masomo yao ya Kemia na Baiolojia kwa kujipatia zawadi hizo na vyeti kwani ni jambo linalowajenga kisaikolojia na kuwapa moyo katika masomo yao.
Amesema wao kama wawakilishi wa vyuo mbalimbali na wadau wa elimu hapa nchini wataweza kutoa ushauri kwa wasomi hao hasa wanapofikia wakati wa kuingia katika elimu ya juu na ushauri wao utakuwa ni wapi wanaweza kusoma kwa Ufadhili (Scholarship) ama kwa gharama nafuu, Kipi cha kusoma au taaluma ipi wanayoweza kusomea yenye soko katika ajira au mahitaji ya nchi.
Tunajua nje ya nchi kuna vyuo vinavyotoa elimu nzuri na vyenye teknolojia ya hali ya juu katika kufundisha masomo mbalimbali ikiwemo huduma bora kabisa kwa wanafunzi na tunaweza kuwatafutia lakini hasa kwa wanafunzi ambao tayari wamejitambua
Tunawaalika Wanafunzi hao kwa makundi, binafsi ama walimu wao katika shule wanazotoka ama wazazi wao watuone kwa maelezo zaidi na ushauri juu ya kufanikisha jambo hili katika kujiunga na vyuo hivyo kama wanahitaji (AUL) tunapatikana jijini Dar es salaam Mlimani City jengo la TCU Complex ghorofa ya saba , Jengo la Benjamin Mkapa Ghorofa ya kwanza kwa mikoani ni Arusha Njiro Copmlex ghorofa ya kwanza na Kenyata Raroad, Mwanza
Post a Comment