GGM NA TACAIDS KUZINDUA KAMPENI YA KILL CHALLENGE MWAKA 2017
Na James Bayachamo-Salvanews
Wito umetolewa kwa wadau Mbali mbali kushirikiana katika mapambano dhidi ya maambukuzi ya ugonjwa wa ukimwi kwa kuungana kwa pamoja katika kampeni ya kili challenge kuhakikisha maambukizi ya ugonjwa huo hayaendelei hapa nchini.
Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na makamo wa rais na miradi endelevu wa mgodi wa dhahabu wa geita (GGM) Simon Shayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa kampeni ya kili challenge kwa mwaka 2017 unaotarajia kuzinduliwa Leo jioni jijini Dar es salaam.
Shayo amesema kuwa kampeni hiyo inayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya VVUna UKIMWI ambayo hufanyika kila mwaka kwa wadau mbali mbali kupanda mlima Kilimanjaro na kuendesha baiskeli kuzunguka mlima huo huku akiongeza kuwa changamoto za kijamii ni changamoto za sekta binafsi pia ndiyo maana (GGM) wameamua kushirikiana na tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) katika mapambano hayo kwa takribani miaka 16 sasa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt Leonard Maboko ameishukuru kampuni ya (GGM) kwa harakati zake dhidi ya VVU na Ukimwi huku akiongeza kuwa mapambano dhidi yake siyo ya mtu mmoja mmoja Bali ni ya watanzania wote na sekta mbali mbali zikiungana kwa pamoja hatua hiyo itachangia maambukizi ya Ukimwi kupungua mpaka kufikia asilimia 0.3 mwaka 2030 huku akiitaja mikoa ya Njombe,Iringa na Mbeya kama vinara wa maambukizi ya VVU.
Post a Comment