EAC KUANGALIA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA KWA NCHI WANACHAMA
Jumuiya ya afrika ya mashariki (EAC) inatarajia kuangalia changamoto za kibiashara kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa lengo la kuzifanyia ufumbuzi.
Akizungumza leo jijini dar es salaam na waandishi wa habari, Kamishina mkuu wa forodha wa jumuiya hiyo Quandiyay Akonaay amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho wanatarajia kuingia kwenye mpango wa awamu ya pili ya maazimio ya mabadiliko ya maendeleo ya forodha katika soko la afrika ya mashariki kumekuwa na urahisishaji kwa wafanya biashara waliorasimishwa ili kupata huduma bora
Aidha amesema kuwa kwa sasa wako kwenye utekerezaji wa mipango mbalimbali ya forodha ambayo ina lengo la kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa faida ya wafanya biashara waliopo katika nchi wanachama hivyo bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizi hupita kwa uangalizi maalumu na ukaguzi wa hali ya juu kutoka nchi moja kwenda nyingine .
Naye Kamishna wa Forodha Nchini Uganda, Dickson Kateshumbwa amesema kuwa mkutano wa Umoja wa Forodha kwa nchi zilizo kwenye uanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki hufanyika kwa zamu nchi zote za uanachama. Ambapo kwa mwaka huu mkutano huo umefanyika hapa nchini Tanzania na kila mwaka mkutano huo hufanyika katika ngazi tatu, ambazo ni ngazi zinayohusisha wataalamu wa masuala ya forodha ambao hutoka katika mamlaka za mapato za kila nchi wanachama,
Mkutano huo ulianza Aprili 21 mwaka huu na umemalizika leo Aprili 27 ambapo maazimio mbalimbali juu ya mkutano huo yamejadiliwa na miongoni mwa hayo ni, mpango wa kuwa na himaya moja ya forodha, muunganiko wa huduma za kiforodha na mapitio ya viwango vya ushuru na kanuni za uasili wa bidhaa.
Na James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment