Header Ads

header ad

DAWASCO WATAKIWA KUWAFIKIA WANANCHI


 

Na James Salvatory
Wito umetolewa kwa watendaji wa Mamlaka ya Maji safi Jijini Dar es
Salaam (DAWASCO) kuongeza nguvu katika usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi kuliko kuwekeza katika Uzalishaji kama ilivyo sasa.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo wakati wa alipotembelea ofisi za Dawasco na kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo, ambapo amewataka kuongeza kasi katika usambazaji wa Maji na kuboresha miundombinu.

Aidha Profesa Mkumbo ametoa rai kwa Taasisi zisizolipia huduma hiyo
kusitishiwa mara moja kama ambavyo Agizo la Rais Magufuli kwa wasiolipia huduma ya Umeme kusitishiwa huku akiwataka  waanze kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na utunzaji wa maji pamoja na vyanzo vyake ili kuzuia upotevu wa maj.

Awali akiwasilisha ripoti ya hali ya utoaji huduma wa Mamlaka hiyo
Mkurugenzi Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kwa sasa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani changamoto ya Huduma za maji safi zimepungu

Powered by Blogger.