Header Ads

header ad

JUMIA WAJA NA MFUMO MPYA WA MANUNUZI KWA NJIA YA MTANDAO.



 Meneja masoko wa kampuni ya JUMIA TANZANIA,ALBANY JAMES akizungumza na wanahabari hawapo pichani.


  Afisa mkuu wa biashara Jumia Tanzania,MIKOLAG KUCIA akizungumza na wanahabari [hawapo pichani}na wana habari namna malipo yanavyofanyika hasa pale mtu anapopokea bidhaa mara baada ya kuiagiza mtandaoni.





Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali   nchini wakimsikiliza Afisa mkuu wa biashara Jumia Tanzania,MIKOLAG KUCIA [hawapo pichani}akiwaelezea namna malipo yanavyofanyika hasa pale mtu anapopokea bidhaa mara baada ya kuiagiza mtandaoni.




Kampuni inayojihusisha na kutoa huduma ya manunuzi ya bidhaa kwa njia mtandao  ya JUMIA TANZANIA imeboresha huduma zake kwa kuja na mfumo mpya ujulikanayo kama  CASH ON DELIVERED [COD]ambayo itawawezesha wateja wanaogiza bidhaa kupuitia tovuti ya Jumia Tanzania kulipia bidhaa mara baada ya bidhaa hizo kuwafikia.
À
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam meneja masoko wa Jumia Tanzania,ALBANY JAMES amesema kuwa mfumo huo mpya utawajengea uaminifu wateja wanaonunua bidhaa kupitia mtandao kujenga uaminifu kwa huduma zote za manunuzi wanazozifanya kwa njia ya mtandao.

‘’jumia Tanzania tunayo furaha kuwajulisha wateja wetu wote kwamba hivi sasa wanaweza kulipia bidhaa zao wanazozinunua kwa njia ya mtandao pindi bidhaa zinapowafikia na tumeona ni vyema kuwapa wateja wetu chaguo hilo kwa kulipia bidhaa baada ya kuziona kwa macho na kujiridhisha kwani huduma ya manunuzi kupitia mtandao ni ngeni kwa watanzania walio wengi jambo linalofanya engi wao kuwa na hofu na kudhani wanatapeliwa’’alisema Bw JAMES
Akizungumzia faida za mfumo huo mpya Bw James amesema mbali na mteja kuionana kujiridhisha na bidhaa aliyoiagiza kabla ya kufanya malipo pia mteja atapata fursa ya kuweza kubadilisha bidhaa endapo hatoridhika nayo na kumfanya mteja kuchagua kulipia fedha kwa njia ya mtandao ama pale bidhaa itakapomfikia.

“ningependa kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia ofa mbali mbali za manunuzi ya bidhaa kupitia tovuti yetu au mitandao ya kijamii ya Facebook,Twitter na Instagram lakini pia wafanyabiashara wa kitanzania kuhamia kwenye njia za mitandao ili kupanua wigo kwa wateja wao kuna faida nyingi za kujiunga na Jumia Tanzania ikiwemo kujiongezea wateja wengi tofauti na wale wanaotembelea maduka yao moja kwa moja’’aliendelea kuelezea Bw JAMES
Jumia Tanzania ambayo imeanza kazi zake rasmi hapa nchini miaka miwili iliyopita imefanikiwa kutanua wigo wa biashara za mtandaoni kwa kuwawezesha watanzania wengi kununua bidhaa mbali mbali kutoka katika maduka na kampuni mbali mbali kupitia mitandao jambo ambalo limekuza teknolojia hiyo ambayo inawapa urahisi wateja kununua bidhaa bila kuzifuata madukani.



No comments

Powered by Blogger.